Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:44

Hatma ya Barasa kwenda ICC kujulikana leo Kenya


Fatou Bensouda,mwendesha mashtaka mkuu wa ICC huko The Haque
Fatou Bensouda,mwendesha mashtaka mkuu wa ICC huko The Haque
Mahakama moja nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi Ijumaa juu ya ombi la mahakama ya kimataifa ya uhalifu- ICC kutaka kukabidhiwa kwa mwanaharakati Walter Barasa. Mahakama hiyo yenye makao makuu yake The Haque inamshutumu mtu huyo kwa kuingilia mashahidi.

Barasa anakanusha shutuma hizi kuwa hazina msingi. “Sina wasi wasi kwa sababu ninakanusha shutuma zilizoelezewa dhidi yangu, na zaidi ya hayo wakili wangu ana maelezo na ataelezea hilo wakati ukifika, alisema Barasa”.

ICC ilitoa kibali cha kukamatwa dhidi ya Barasa lakini aliwasilisha changamoto dhidi ya amri ya kukamatwa katika mahakama ya Kenya. Wakili wa upande wa utetezi wa Barasa, Kibe Mungai aliishutumu ICC kwa kudharau katiba ya Kenya. Anasema kwa mfano kesi yake inatakiwa kusikilizwa katika mahakama za Kenya, na pia kwamba hatua ya ICC inakiuka haki yake ya katiba ya kuona ushahidi dhidi yake.

Walter Barasa
Walter Barasa


“Bwana Barasa anataka mahakama itangaze kwamba serikali ya Kenya haiwezi kutekeleza ombi la ICC”, alisema Mungai. “Kama akifanikiwa huo ndio mwisho wa habari. Kama pia anafanikiwa kwa upande mwingine kwamba kesi ifanyike nchini Kenya, basi suala la hati ya kukamatwa linafikia tamati. Kama hatoshinda basi huwenda akajisalimisha kwa ICC”.

Mungai anasema kama mahakama inafuata katiba ya Kenya mteja wake hastahili kukabidhiwa kwa ICC. Alisema wote ICC na Kenya walikosea walipotoa hati ya kukamatwa kwa Barasa.“Tuna nafasi nzuri”, alisema Mungai. “ICC imekuwa ikishughulikia suala hili kinyume cha sheria na Kenya kama taifa imeitafsiri vibaya sheria katika kutoa ombi la kutaka ajisalimishe”.

ICC ilimshutumu Barasa kwa kuwahonga mashahidi katika kesi ya Naibu Rais wa Kenya, William Ruto. Mahakama inamshutumu bwana Ruto na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kuwa wahusika wakuu katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya wa mwaka 2007-2008 ambazo zilisababisha kiasi cha watu 1,300 kufariki na maelfu kukoseshwa makazi ndani ya nchi. Barasa anakanusha mashtaka ya ICC.

Wakili wa upande wa utetezi, bwana Mungai anasema hati ya kukamatwa iliyotolewa na ICC dhidi ya Barasa inakiuka katiba ya Kenya.
XS
SM
MD
LG