Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:02

Hali yazidi kuwa tete Syria


Waandamanaji wa Syria waliovalia bendera za nchi yao katika mji wa Homs Desemba 27, 2011
Waandamanaji wa Syria waliovalia bendera za nchi yao katika mji wa Homs Desemba 27, 2011

Mauaji ya wapinzani wa serikali ya Syria yaendelea

Makundi ya kutetea haki za binadamu Syria, yanasema vikosi vya ulinzi vimeuwa watu watano Alhamis huku wafuatiliaji kutoka Jumuiya ya nchi za Kiarabu wakielekea katika maeneo matatu muhimu ambapo serikali yaripotiwa kuwakandamiza sana wapinzani. Baadhi ya wanaharakati wanasema baadhi ya waandamanaji waliouawa walipigwa risasi na majeshi ya serikali katika mji mkuu Damascus. Ghasia za Alhamis zilitokea huku wafuatiliaji hao wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu wakijiandaa kuzuru miji ya Daraa, Hama na Idlib ambako serikali imeahidi kukomesha ukamataji na mauaji ya wapinzani wake ikiwa ni pamoja na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa. Jumatano wanaharakati na makundi ya kutetea haki za binadamu yalisema majeshi ya serikali yameuwa takriban watu 39 tangu wafuatiliaji wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu kuwasili nchini humo Jumatatu ikiwa ni pamoja na watu sita waliouawa katika mji wa Hama.

XS
SM
MD
LG