Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:02

Hali yazidi kudumaa nchini Syria


Baghdad yadai al-Qaida yafanya mashambulizi

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia hali nchini Syria anasema ghasia nchini humo zimefikia kiwango kisichowahi kuonekana na kwamba sharti kuwe na sitisho la mapigano ili timu hiyo iweze kuendelea na kazi yake iliyositishwa mwezi jana. Tamko la meja jenerali Robert Mood Alhamis limetolea huku vikosi vya serikali vikiendelea kupambana na wapinzani kote nchini humo. Naye waziri wa mambo ya nje wa Iraq anasema Baghdad ina ushahidi wa kutosha wa kijasusi kuwa wanamgambo wa al-Qaida wanavuka mpaka na kuingia Syria kufanya mashambulizi. Jenerali Mood amesema jamii ya kimataifa inapaswa na ina wajibu wa kisiasa kwa raia wa Syria na ni sharti ichukue hatua kukomesha ghasia nchini humo.

XS
SM
MD
LG