Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:01

Hakimu akataa kumpa mkuu wa IMF dhamana


Dominique Strauss-Khan akipelekwa rumandi baada ya hakimu kukata kumuachilia kwa dhamana katika mahakama ya uhalfu ya Manhattan
Dominique Strauss-Khan akipelekwa rumandi baada ya hakimu kukata kumuachilia kwa dhamana katika mahakama ya uhalfu ya Manhattan

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa anaendelea kushikiliwa mjini New York kwa mashitaka ya kujaribu kumbaka mwanamke mmoja katika hoteli ya Sofitel.

Hakimu wa Mahakama moja mjini New York alikata ombi la Dominique Strauss-Khan, kuachiliwa huru kwa dhamana, kwa mashtaka ya jaribio la kumbaka mwanamke mmoja msafisha chumba wa hoteli. Hakimu aliamua kwamba Mkuu huyo wa IMF ni mtu anaeweza kusafiri nje ya nchi.

Naibu mwendesha mashtaka John McConnell aliiambia mahakama ya uhalifu ya Manhattan kwamba mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na jaribio la ubakaji.

McConnell alimuomba hakimu Melissa Jackson kukataa kumfungua kwa dhamana, akisema Strauss-Khan ana ushawishi wa kisiasa na rasilmali ya kifedha kumwezesha dhamana ya mamilioni ya dola na kutorudi tena mahakamani.

Mawakili wa Bwana Strauss-Kahn wamependekeza mpango wa kutowa dhamana ya dola milioni moja, na kwamba mkuu huyo wa IMF atabaki nyumbani kwa binti yake New York na kufungwa mkanda wa elektroniki utakaoonesha mahala anapokwenda wakati wote, pamoja na kukabidhi wakuu hati zake zote za usafiri.

Bwana Strauss-Kahn alikamatwa Jumamosi usiku akiwa ndani ya ndege ya shirika la Air France kwa safari ya kwenda Ufaransa. Atarudishwa mahakamani kwa kesi ya awali siku ya Ijumaa.

XS
SM
MD
LG