Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 10:32

Hagel akosa kuidhinishwa kama waziri wa ulinzi


Seneta wa zamani Chuck Hagel
Seneta wa zamani Chuck Hagel

Rais Obama akosoa maseneta wa chama cha Republican kwa siasa za mgawanyiko wakati Marekani ingali vitani Afghanistan.


Maseneta wa chama cha Republican wamezuia kura ya kumthibitisha mteuliwa wa rais Obama, Chuck Hagel kuwa waziri mpya wa ulinzi.

Baraza la Senate lilikosa kura mbili tu Alhamisi kuweza kumwidhinisha Hagel, kufuatia ombi la Wademokrat kumaliza malumbano ya mdahalo wa muda mrefu na maseneta wa chama cha Republican juu ya uteuzi huo na kufikia maamuzi ya mwisho.

Baraza la senate sasa linakwenda kwenye mapumziko ya siku 10 na itambidi bwana Bw. Hagel kusubiri muda huo wote ili kuweza kujua ikiwa atakuwa mkuu ajaye wa Pentagon.

Rais Obama alisema hatua ya maseneta wa chama cha Republican haikutarajiwa. Amesema pia inasikitisha kuona maseneta wakitumia siasa za aina hiyo wakati Marekani ingali vitani huko Afghanistan.

Wabunge wa chama cha Republican wanazuilia kuidhinishwa kwa Bw. Hagel, wakiitaka White House kutoa maelezo zaidi juu ya shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka jana katika ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Benghazi, Libya.

Shambulizi hilo lilimwua balozi wa Marekani Christopher Stevens na Wamarekani wengine watatu. Lakini Ikulu ya Marekani inasema imeshatoa maelezo ya kina kwa bunge juu ya shambulizi hilo.

Rais Obama alimchagua Hagel ambaye zamani alikuwa seneta wa chama cha Republican kuchukua nafasi ya waziri wa ulinzi anayeondoka Leon Panetta.
XS
SM
MD
LG