Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:53

Gwajima, Manji Washikiliwa na Polisi Dar es Salaam


Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania limesema linaendelea kuwashikilia na kuwahoji mfanyabiashara Yusuph Manji na kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo Mchungaji Josephat Gwajima.

Watu hao jana Alhamisi walifika kituo kikuu cha polisi kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Paul Makonda katika sakata linaloendelea la dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema timu maalum ya upelelezi iliyojumuisha vyombo vingine vya usalama inaendelea kuwahoji Manji na Mchungaji Gwajima.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ameripoti kuwa polisi imetangaza kuwatia mbaroni jana watu 11 pamoja na kete 38 za dawa za kulevya na magunia matano ya bangi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:14 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Aidha Kamanda Sirro amesema katika orodha ya watu 65 waliotakiwa hivi karibuni kuripoti kituo cha polisi ni wanne tu ndiyo waliojitokeza ambapo ametoa wito kwa wale wote waliotajwa katika orodha iliyotolewa juzi kujitokeza kwa hiari kabla jeshi hilo halijachukua hatua nyingine.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) leo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma amesema hatakwenda polisi kuhojiwa kama alivyoamuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Mbowe hata hivyo amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ikiwa taratibu sahihi zitafuatwa katika uchunguzi huo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Mbowe pia ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Bwana Makond kwa madai ya kumshushia hadhi kama mbunge na kiongozi wa upinzani bungeni kwa kumhusisha na tuhuma hizo za dawa za kulevya

Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungan wa Tanzania, John Magufuli, leo Februari 10, 2017 amemteua Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (Drug Control and Enforcement Authority).

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Dina Chahali, Tanzania

XS
SM
MD
LG