Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:25

Ghasia zinaendelea Sudan Kuisni watu 80 wauwawa


A Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS wanapiga doria katika mji wa Abyei, Sudan Kusini.
A Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS wanapiga doria katika mji wa Abyei, Sudan Kusini.

Maafisa wa Sudan Kusini wanasema watu 82 wameuwawa wakati wanamgambo walipovamia kundi la wachunga ng’ombe upande wa kusini.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Philip Aguer alisema mapigano yalitokea Jumanne katika jimbo la Warrap. Alisema mapigano yalizuka wakati waasi walipovamia zizi la ng’ ombe na kuuwa watu 34. Amesema baadae wachunga ng’ombe walifanya shambulio la kushtukiza dhidi ya wanamgambo na kuwauwa wote 48.

Katika tukio lingine Jumanne Umoja wa Mataifa umesema walinda amani wanne wa Zambia walipigwa risasi na kujeruhiwa katika eneo lingine la machafuko kaskazini kusini mwa mkoa unaogombaniwa wa Abyei.

Ghasia zimeongezeka Sudan Kusini na kuongeza wasi wasi juu ya utulivu wa eneo hilo wakati linapojitayarisha kujitangazia uhuru kutoka Kaskazini Julai 9.

Mamia ya watu wameuwawa katika mapigano kati ya makundi mbali mbali ya waasi tangu Januari wakati wakazi wa kusini kwa wingi mkubwa walipiga kura kutaka kujitenga kutoka kaskazini.

XS
SM
MD
LG