Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 14:44

Ghasia zazuka Zambia


Kiongozi wa upinzani Zambia Michael "King Cobra" Sata (kati kati) akitoka kwenye kituo cha kupigia kura.
Kiongozi wa upinzani Zambia Michael "King Cobra" Sata (kati kati) akitoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Huku kiongozi wa upinzani akiongoza katika kura zilizohesabiwa mpaka sasa, lakini matokeo kamili yachelewa wananchi wa Zambia waamua kuandamana.

Maandamano yamezuka katika maeneo ya kaskazini na katikati ya Zambia huku wafuasi wa upinzani wakipinga mwendo wa pole wa kuhesabu kura baada ya uchaguzi wa urais Jumanne wiki hii.

Polisi wanasema waandamanaji walivurumishia magari mawe na hata majengo katika miji ya Kitwe na Ndola Alhamisi na kuchoma moto soko la Kitwe.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo Martin Malama aliwaambia waandishi habari kuwa maafisa wake wanajaribu kudhibiti hali hiyo. Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanaonyesha kiongozi wa upinzani Michael Sata anaongoza kwa asili mia 43 ya kura akifuatwa na rais Rupiah Banda kwa asili mia 36 ya kura.

Wafuatiliaji wanasema kutokana na mwendo huo wa pole wa kuhesabu kura haitawezekana kutoa matangazo ya mshindi wa kiti hicho Alhamisi kama ilivyotegemewa.

XS
SM
MD
LG