Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:25

Ghasia zazuka Sudan


Wanawake wa Sudan wakicheza na silaha zao wakishiriki katika zoezi la kijeshi kuonesha nguvu zao wakati wa ziara ya balozi wa UNICEF Mia Farrow mjini Gallap.
Wanawake wa Sudan wakicheza na silaha zao wakishiriki katika zoezi la kijeshi kuonesha nguvu zao wakati wa ziara ya balozi wa UNICEF Mia Farrow mjini Gallap.

Maafisa wa jeshi wanasema waasi wanaomuunga mkono mwanajeshi aliyeasi Peter Gadet walishambulia majeshi katika tarafa ya Mayom.

Jeshi la Sudan Kusini linasema mapigano na wanamgambo wa waasi katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity yamesababisha vifo vya wanajeshi 20.

Maafisa wa jeshi wanasema waasi wanaomuunga mkono mwanajeshi aliyeasi Peter Gadet walishambulia majeshi katika tarafa ya Mayom Jumanne .

Mapigano hayo ni ghasia za mwisho tangu wananchi wa Sudan Kusini walipopiga kura kwa wingi mkubwa kuchagua kujitenga na kaskazini katika kura ya maoni ya January.

Chama tawala cha Sudan kusini kimeishutumu serikali ya Kaskazini ya Khartoum kwa kuwafundisha na kuwapa silaha wanamgambo ili kuzusha vurugu Sudan Kusini na kuwapindua uwongozi wa kusini kabla ya kujitenga rasmi July. Khartoum iinakanusha madai hayo.

Wakati huo huo mamia ya wasudan kutoka kwenye jimbo lenye mzozo la Darfur wamefanya maandamano madogo katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi .

Mashahidi wanasema vijana waliokuwa wakiandamana walikusanyika Jumatano katika miji kadhaa ya kaskazini ikiwa ni pamoja na mji mkuu Khartoum na Darfur.

Katika mji mkuu mashahidi wanasema kiasi cha wanafunzi 100 kutoka chuo kikuu cha al- Nilein waliandamana nje ya majengo ya chuo kabla vikosi vya usalama hawajaanza kuwakamata.

Katika mji wa Dleng, jimbo la Kordofan ya Kusini mashahdi wanasema polisi walifyetua mabomu ya kutowa machozi kuwatawanya zaidi ya wanafunzi 100.

XS
SM
MD
LG