Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:06

Ghasia za sababisha uharibifu wa mali Zanzibar


Tairi zinawaka mpta katika njia moja kuu Zanzibar kufuatia ghasia zilizosababishwa na wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho
Tairi zinawaka mpta katika njia moja kuu Zanzibar kufuatia ghasia zilizosababishwa na wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohamed Aboud, ametoa taarifa kuhusiana na ghasia akisema walosababisha uharibifu wa mali watachukuliwa hatua.

Hali ya utulivu imeripotiwa katika kisiwa cha Unguja Jumapili usiku, kufuatia ghasia na uharibifu wa mali mwishoni mwa wiki baada ya maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho.

Hata hivyo mwandishi wetu mjini Zanzibar Munir Zacharia anaripoti kwamba kuna vizuizi katika njia muhimu za kisiwa hicho na watu wamebaki nyumbani, na haijulikana hali itakuwa vipi siku ya Jumatatu watu wakirudi kazini

Kanisa lililotiwa moto
Kanisa lililotiwa moto

Ghasia zilizuka Jumamosi baada ya wanaharakati wa kundi hilo kutaka kushambulia makao makuu ya polisi kufwatia kukamatwa kwa imam wa msikiti wa Biziredi ambaye ni mmoja kati ya wa viongozi wa Uamsho, Sheik Mussa AliJuma.

Mohamed Aboud waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa rais
Mohamed Aboud waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa rais

Taarifa ya serikali Jumapili jioni na waziri wa nchi katika afisi ya makamu wa pili wa rais Mohamed Aboud, imeeleza kwamba kwa wakati huu mikutano yote ya hadhara na maandamano
ambayo hayajapata kibali cha polisi yamepigwa marufuku.

Maafisa wa usalama wanachukua hatua zinaozhitajika kudumisha tena usalama na
amani. Bado haijulikani kama kiongozi huyo wa Uamsho, atafunguliwa mashtaka
au atafikishwa mahakamani Jumatatu.

Uamsho umetoa taarifa ikidai kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Taarifa hiyo inatoa wito kwa Wa Zanzibari kuendelea
kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu.


XS
SM
MD
LG