Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 02:27

Ghailani apewa kifungo cha maisha


Mwendesha mashitaka wa serikali Nicholas Lewin, akitoa maelezo mbele ya mahakama katika kesi ya Ghailani mjini New York.
Mwendesha mashitaka wa serikali Nicholas Lewin, akitoa maelezo mbele ya mahakama katika kesi ya Ghailani mjini New York.

Mtanzania Ahmed Ghailani aliyekutwa na hatia ya kosa moja katika shambulizi la mabomu la ubalozi wa Marekani mjini Dar es salaam mwaka 1998 amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama moja ya New York.

Mawakili watetezi wa Ghailani, mwenye umri wa miaka 36, waliiomba mahakama kumhurumia kwa sababu hakujua kikamilifu kuhusu shambulizi hilo, na kwamba aliteswa akiwa mikononi mwa CIA.

Lakini Jaji Lewis Kaplan wa mahakama ya serikali kuu New York alitupilia mbali ombi hilo, akisema kuwa vyovyote alivyoteseka Ghailani sio sawa na mateso aliyosababisha yeye pamoja na wenzake.

Waendesha mashitaka walisema mahakamani kuwa kifungo cha maisha kinastahili kwa sababu Ghailani alijua wakati wote kuhusu shambulizi hilo na alikuwa mmoja wa watendaji wakuu wa kitendo hicho.

Ghailani alikutwa na hatia katika kosa moja la kula njama za kuharibu majengo ya serikali ya Marekani katika mashambulizi mawili ya pamoja katika balozi za Marekani Dar es salaam na Nairobi. Alikutwa hana hatia katika mashitaka mengine 224 ya mauaji na mashitaka mengineyo.

XS
SM
MD
LG