Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:13

Mjumbe wa UM anasema mkataba wa Darfur unahitajika haraka


Ujumbe wa UM unakutana na wanawake katika kambi ya watu waloipoteza makazi yao ya Abu Shouk nje kidogo na mji mkuu wa Darfur wa El Fasher.
Ujumbe wa UM unakutana na wanawake katika kambi ya watu waloipoteza makazi yao ya Abu Shouk nje kidogo na mji mkuu wa Darfur wa El Fasher.

Ibrahim Gambari mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa huko Darfur, anaongoza pia operesheni kubwa kabisa kwa wakati huu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa afrika UNAMID huko Darfur nchini Sudan. Operesheni hiyo ina zaidi ya wanajeshi, polisi na watumishi wa kiraia 25,000.

Akizungumza na VOA, juu ya atahri za kura ya maoni inayotarajiwa kufanyaika huko Sudan ya Kusini hapo Januari 9, Profesa Gambari anasema, kura hiyo tayari ina atahri kubwa katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa ugomvi wa Darfur kwa sababu baadhi ya viongozi wa makundi ya waasi wanafikiria kuwa iwapo upande wa Kusini utaamua kujitenga, basi serikali ya Khartoum itakuwa dhaifu na huenda wakafikia makubaliano yatakayowaridhisha wao.

Lakini mwakilishi wa Umoja wa Mataifa hakubaliani na wazo hilo, kwani anasema ikiwa kutakua na serikali dhaifu Khartoum hiyo haimanishi kwamba serikali hiyo haitoweza kuchukua maamuzi magumu katika kutanzua sababu msingi za ugomvi wa Darfur.

XS
SM
MD
LG