Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:29

Gadhafi anusurika katika shambulizi la NATO


Maafisa wa Libya wakiangalia eneo la nyumba inayosemekana kushambuliwa na NATO mjini Tripoli Jumamosi, April 30,2011
Maafisa wa Libya wakiangalia eneo la nyumba inayosemekana kushambuliwa na NATO mjini Tripoli Jumamosi, April 30,2011

Libya yasema shambulizi hilo limeuwa mmoja wa watoto wa Gadhafi, Saif al-Arab Gadhafi

Kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi amenusurika katika shambulizi la anga lililofanywa na majeshi ya NATO na kuuwa mmoja wa watoto wake na wajukuu wake watatu.

Msemaji wa serikali ya Libya Moussa Ibrahim alitangaza vifo hivyo Jumamosi katika mkutano na waandishi wa habari. Alisema Saif al-Arab Gadhafi mwenye umri wa miaka 29 na wajukuu watatu wa Gadhafi waliuawa katika kile alichoita jaribio la moja kwa moja kumwua kiongozi huyo wa Libya. Ibrahim alisema mtoto huyo wa Gadhafi alikuwa mwanafunzi.

Ibrahim anasema Bw Gadhafi na mkewe walikuwa ndani ya nyumba ya mtoto wao huyo wakati wa shambulizi hilo lakini hawakudhurika. Hata hivyo, alisema watu wengine kadha katika nyumba hiyo walijeruhiwa.

Waandishi wa habari walichukuliwa katika nyumba hiyo na kuonyeshwa uharibifu uliofanyika kutokana na shambulzi hilo. NATO haijatoa tamko lolote la mara moja kuhusu shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG