Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:30

G20 yakubaliana kudhibiti bei ya vyakula


Waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner
Waziri wa fedha wa Marekani Timothy Geithner

Mawaziri wa kilimo wa G20 wakubaliana juu ya hatua za kudhibiti bei ya vyakula

Viongozi wa nchi 20 zenye nguvu za kiuchumi wamekubaliana Alhamis juu ya hatua za kudhibiti bei ya juu ya vyakula duniani. Mawaziri wanaohusika na kilimo kutoka kundi la G20 walikutana kwa mara ya kwanza Jumatano na Alhamis mjini Paris Ufaransa, kufuatia mwaka wa mazungumzo yaliyokumbwa na utata na hatimaye kukubaliana juu ya hatua kadhaa za kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula.

Mawaziri hao pia walitoa mwito kuwe na sheria za kudhibiti masoko ya kifedha. Lakini wataalam wengi wanasema kutokuwa na uhakika juu ya hali ya baadaye kumechangia ongezeko la bei ya vyakula katika miaka ya karibuni. Inategemewa mawaziri wa kifedha kutoka nchi hizo 20 zenye nguvu za kiuchumi watatoa maelezo zaidi juu ya makubaliano ya Alhamis.

Mawaziri hao wa kilimo pia walikubaliana kuunda mfumo mpya wa kupashana habari juu ya hifadhi ya chakula na matumizi yake duniani. Rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick alisema hili lilitokana na namna bei ya vyakula ilivyoyumbayumba katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Makubaliano ya Paris yanajumwisha mipango ya kuhifadhi vyakula vidogo vidogo vya kutumia wakati wa dharura katika kanda mbalimbali vinavyoweza kusimamiwa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Lakini utafiti wa Umoja wa Mataifa juu ya chakula mwaka huu unaonyesha kuwa hali mbaya ya hewa ilipunguza uzalishaji wa mahindi na ngano na kwamba gharama kubwa ya mafuta na chumi zinazodumaa zinategemewa kuendelea kuathiri bei ya vyakula na hivyo kupatikana kwa gharama ya juu katika miaka ijayo.

XS
SM
MD
LG