Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:41

Majivu ya mwili wa rais wa zamani wa Cuba yazikwa

Magari ya kijeshi yaliyobeba majivu ya Fidel Castro
Magari ya kijeshi yaliyobeba majivu ya Fidel Castro

Sherehe za maziko katika kisiwa cha Sant Ifigenia huko Santiago de Cuba zilikuwa kwa ajili ya watu maalumu katika dakika za mwisho hivyo kuzuiya waandishi wa habari wa kimataifa waliofika kutoka maeneo mbalimbali kushuhudia ibada ya mazishi.

Mabaki ya kiongozi wa zamani wa Cuba Fidel Castro yamezikwa mashariki mwa nchi hiyo mapema Jumapili asubuhi baada ya siku tisa za maombolezo kote kuzunguuka kisiwa hicho.

Sherehe za maziko katika kisiwa cha Sant Ifigenia huko Santiago de Cuba zilikuwa kwa ajili ya watu maalumu katika dakika za mwisho hivyo kuzuiya waandishi wa habari wa kimataifa waliofika kutoka maeneo mbalimbali kushuhudia ibada ya mazishi.

Castro ambaye kwa kiasi fulani alifurahiwa na baadhi ya raia wa Cuba kwa kuwa mtetezi wa masikini na kukosolewa na wengine kama kiongozi aliyeharibu uchumi wa nchi na kukiuka haki za binadamu , alifariki Novemba 25 akiwa na umri wa miaka 90 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Majivu ya Fidel Castro yaliwasili Jumamosi mchana huko Santiego de Cuba mji ambao alianzia mapinduzi ya Cuba mwaka 1953. Majivu hayo yalihifadhiwa katika boxi la mbao na kuwekewa bendera ya Cuba na kuzingirwa na kioo huku yakiwa yamebebwa na gari la jeshi aina ya jeep kutoka Havana. Maelfu ya raia wa Cuba waliomboleza kifo chake , kwa kufurahi au kuhuzunika wakiwa wamejipanga kwenye mitaa wakati gari hilo likipita.

Rais wa Cuba Raul Castro aliwaambia maelfu ya watu kwamba serikali itaheshimu mapendekezo ya kaka yake kwamba kusiwepo na maeneo au mitaa itakayopewa jina lake.

XS
SM
MD
LG