Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:42

FBI yagundua baadhi ya barua pepe za Clinton


Mgombea urais wa Democrat, Hillary Rodham, akiwa kwenye moja ya kampeni zake katika jimbo la New Hampshire
Mgombea urais wa Democrat, Hillary Rodham, akiwa kwenye moja ya kampeni zake katika jimbo la New Hampshire

Maafisa wa Marekani walisema kwamba wachunguzi walipata barua pepe binafsi na nyingine zinazohusiana na kazi ambazo zinaaminika kuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje, Hilllary Clinton alizifuta kutoka kwenye kifaa alichokuwa akikitumia wakati akihudumu kama mwanadiplomasia wa cheo cha juu nchini Marekani kutoka mwaka 2009 hadi 2013.

Idara ya upelelezi ya serikali kuu Marekani-FBI, imesema jinsi nyaraka ambazo zilitajwa kuwa ni za usalama wa taifa zimeishia kwenye barua pepe binafsi ya bibi.Clinton.

Bibi. Clinton, hivi sasa ni mgombea anayeongoza anayewania uteuzi wa urais kwa Democrat mwaka 2016 alisema alitumia barua pepe binafsi kwa mawasiliano rahisi hivyo basi hakuwa na haja ya kuhodhi akaunti mbili za barua pepe, moja ikiwa ya kikazi katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani na nyingine kwa ajili ya masuala yake binafsi.

Haikufahamika vyema ni barua pepe ngapi zimegundulika katika kifaa hicho kilichokuwa na barua pepe 60,000. Bibi. Clinton alisema barua pepe hizo zilifutwa lakini mchunguzi mmoja aliliambia gazeti la The New York Times kwamba haikuwa vigumu kuzipata barua pepe hizo.

Hillary Clinton, mgombea urais anayeongoza wa Democrat
Hillary Clinton, mgombea urais anayeongoza wa Democrat

Bibi.Clinton alisema kwamba barua pepe 30,000 kati ya hizo zilikuwa na maelezo binafsi alizifuta na nakala zilizobaki ziliwasilishwa kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani. Maafisa huko walichunguza kila kitu na waligundua darzeni ya nakala, japokuwa Clinton alisema ana uhakika kwamba hakuna barua pepe yeyote iliyokuwa na alama ya siri wakati alipotuma au kupokea.

Wizara ya mambo ya nje nchini Marekani ilitoa barua pepe kadhaa za kiofisi na inapanga kutoa zaidi katika wiki kadhaa zijazo. Barua pepe hizo zilizopatikana kwenye kifaa hicho hatimaye zitawekwa hadharani.

XS
SM
MD
LG