Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:13

EU yazindua miradi ya kupambana na ugaidi duniani


Katibu mkuu wa Arab League, Nabil Al-Araby (L) akipeana mkono na mkuu wa masuala ya nje wa EU,Federica Mogherini huko Brussels, Jan. 19, 2015.
Katibu mkuu wa Arab League, Nabil Al-Araby (L) akipeana mkono na mkuu wa masuala ya nje wa EU,Federica Mogherini huko Brussels, Jan. 19, 2015.

Umoja wa Ulaya-EU unazindua miradi mipya ya kupambana na ugaidi na nchi za ki-Islam na inaongeza ushirikiano wake wa kijasusi baada ya mashambulizi yaliyosababisha vifo nchini Ufaransa na mapambano ya ghasia huko Ubelgiji.

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU walikutana jumatatu mjini Brussels na katibu mkuu wa Arab League, Nabil Elaraby. Baada ya hapo mkuu wa masuala ya mambo ya nje wa EU, Federica Mogherini alisema EU itashirikiana taarifa juu ya washukiwa magaidi na uwezekano wa mashambulizi na nchi nyingi kote katika dunia ya kiarabu, Afrika na Asia.

“Tulichukua uamuzi ndani ya baraza la mambo ya nje kuratibu katika njia nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa hadi hivi sasa. Kwanza kabisa, kwa jitihada za kushirikiana taarifa, taarifa za kijasusi, sio tu ndani ya Umoja wa Ulaya lakini pia na nchi nyingine zinazotuzunguka, kuanzia kutoka Mediterranean na dunia ya kiarabu, kuanzia kutoka Uturuki, Misri, nchi za ghuba, Afrika kaskazini, lakini pia tukiangalia zaidi Afrika na Asia kwa wakati fulani fulani”.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Philip Hammond
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Philip Hammond

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Philip Hammond alisema ulaya ina azma ya kufanya kilicho muhimu ili kuendelea kuliweka salama bara hilo. Alisema maafisa wanaangalia njia bora za kufuatilia harakati za uwezekano wa magaidi ikiwemo kushirikiana orodha za abiria wanaosafiri kwa ndege.

Kwa upande mwingine mawaziri wa EU walisema watakata rufaa kwa uamuzi wa mahakama moja mwezi uliopita ambao uliliondoa kundi la ki-Islam la wapalestina la Hamas kutoka kwenye orodha ya kigaidi ya EU. Hamas ilihusika katika vita vikali vya siku 50 na Israel mwezi Julai na Agosti mwaka jana.

Sehemu kubwa ya ulaya bado ina wasi wasi na iko kwenye tahadhari ya juu wakati waziri wa sheria wa Ubelgiji aliposema mshukiwa aliyepanga shambulizi la ugaidi lililoshindikana la wiki iliyopita bado anatafutwa.

XS
SM
MD
LG