Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:49

EU yatakiwa kusaidia tatizo la usafirishaji haramu wahamiaji


Meli ya Italy ya walinzi wa pwani pamoja na helikopta wakati wa operesheni ya kuwaokoa wahamiaji, April 19, 2015.
Meli ya Italy ya walinzi wa pwani pamoja na helikopta wakati wa operesheni ya kuwaokoa wahamiaji, April 19, 2015.

Waziri Mkuu wa Italy, Matteo Renzi alisema umoja wa ulaya lazima usaidie katika tatizo la kukabiliana na usafirishaji haramu wahamiaji katika mataifa ya ki-Afrika baada ya wahamiaji wapatao 900 kuzama Jumapili wakati boti yao ilipozama kwenye bahari ya Mediterranean.

Bwana Renzi alitoa matamshi hayo Jumatano wakati akizungumza na wabunge wa Italy mjini Rome siku moja kabla ya viongozi wa ulaya kukutana kwa kikao cha dharura kuzungumzia matatizo hayo. Wabunge pia waliomboleza kwa kukaa kimya kuwakumbuka watu waliofariki kutokana na ajali hiyo.

Kundi la haki za binadamu la Save the Children liliripoti Jumatano kwamba lilipata taarifa kwamba watoto wadogo wapatao 60 walikuwa ndani ya boti wakati ilipozama na kundi linaonya kwamba kama hali hii ya sasa inaendelea watoto wahamiaji wasiopungua 2,500 wataweza kufariki katika ajali kama hizo kwenye bahari ya Mediterranean mwaka huu.

Kundi la haki za binadamu la Save the Children
Kundi la haki za binadamu la Save the Children

Save the Children ilieleza kwamba wavulana wane ambao wanasema wanaumri chini ya miaka 18 walinusurika kutoka ajali ya Jumapili wakati kapteni wa boti ya wahamiaji hao kwa bahati mbaya alipogonga boti kwenye meli ya mizigo iliyokua inaelekea kuwaokoa.

Waendesha mashtaka wa Italy katika mji wa Sicilia wa Catania walisema kapteni wa boti hiyo raia wa Tunisia aliongoza boti hiyo iliyojaa watu kupita kiasi hadi meli ya kontena ya Ureno muda mfupi kabla ya kuzama nje ya pwani ya Libya siku ya Jumamosi usiku April 18 mwaka 2015. Maafisa wanasema hiyo ni ajali mbaya kabisa iliyosababisha vifo vingi kuwahi kutokea katika bahari ya Mediterranean. Kuna watu 28 pekee walionusurika.

Mwendesha mashtaka ameondowa lawama zozote za uwajibikaji kwa meli hiyo ya mizigo.

XS
SM
MD
LG