Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:03

Erritrea yakanusha kuwapelekea Alshabab silaha.


Wapiganaji wa Alshabab wakiwa mitaani huko Mogadioshu.
Wapiganaji wa Alshabab wakiwa mitaani huko Mogadioshu.

Wizara ya mambo ya nje ya Erritrea yakanusha kupeleka ndege mbili zenye silaha Somalia.

Eritrea imekanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba ilituma ndege mbili zilizojaa silaha kwa wanamgambo wa alshabab huko Somalia Kusini.

Wizara ya mambo ya nje ya Eritrea ilitoa taarifa leo kuwa madai hayo ni “uzushi mtupu”. Wizara hiyo ilikanusha kuwa imepeleka silaha kwa kundi hilo lenye mahusiano na alqaeda na kusema ripoti hiyo ilikuwa ni sehemu ya kampeni ya kutoa taarifa za uongo ili kuihujumu Eritrea.

Jana jeshi la Kenya lilisema limethibitisha kuwa ndege mbili zilitua kwenye mji wa kusini wa Somalia wa Baidoa zikibeba silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa wanamgambo hao wa Alshabab.

Msemaji wa jeshi la Kenya Emmanuel Chirchir hakusema nani alipeleka silaha lakini taarifa za vyombo vya habari zililaumu Eritrea.

XS
SM
MD
LG