Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:56

Elizabeth Taylor afariki kutokana na matatizo ya moyo


Elizabeth Taylor katika mchezo wa Cleopatra.
Elizabeth Taylor katika mchezo wa Cleopatra.

Mchezaji mkongwe wa filamu, Elizabeth Taylor, mashuhuri zaidi kwa filamu yake ya Cleopatra, na urembo wake amefariki mjini LOs Angeles akiwa na umri wa miaka 79

Nyota huyo wa filamu za Hollywood anaripotiwa alifariki katika hospitali ya Cedars-Sinai kutokana na matatizo ya moyo baada ya kulazwa huko kwa miezi miwili iliyopita jijini Los Angeles.

Taylor alianza kuwa mashuhuri akiwa na umri wa miaka 12, na mara nyingi alikuwa akitajwa kama mwanamke mrembo duniani.

Mara yake ya mwisho kucheza katika filamu ilikua 2001 katika michezo kadhaa ya kuigiza kwenye televisheni ya Marekani. Uhodari wake ulimsababisha kupokea mara mbili tunzo ya juu ya wachezaji filamu marekani, Oscar kwa michezo ya "Butterfield 8", mwaka 1960 na "Who's afraid of Virginia Woolf" mwaka 1966.

Hata hivyo umashuhuri wake unatokana zaidi na ukarimu wake, mashabiki wake, hali ya maisha yake akiwa ameolewa mara saba. Taylor alitumia umashuhuri wake kuchangisha fedha kupambana na HIV ukimwi akianzisha shirika lake binafsi la Elizabeth Taylor HIV/Aids Foundation 1991, na kupelekea kuanzishwa kwa taasisi ya utafiti wa ukimwi ya marekani.

XS
SM
MD
LG