Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:56

Ebola yarudi tena Uganda


Ноу Камп
Ноу Камп
Maafisa wa afya nchini Uganda wanasema virusi vya ugonjwa wa Ebola vimesababisha vifo vya watu wawili ikiwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya Shirika la Afya Duniani-WHO kusema ugonjwa wa Ebola umekwisha nchini humo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:58 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Waziri wa afya wa Uganda, Christine Ondoa aliwaambia waandishi wa habari Alhamis kwamba watu wawili kutoka familia moja walikufa kutokana na ugonjwa huo katika wilaya ya Luwero kiasi cha kilomita 50 kutoka mji mkuu Kampala.

Alisema taasisi ya utafiti wa virusi nchini Uganda ilithibitisha hilo na iliongeza kwamba watu watano zaidi walioshukiwa kuwa na mawasiliano na waathirika wanaangaliwa kwa karibu.

Picha ya video kutoka hospitali moja ya Uganda ilionesha watu wakiwa wamelala vitandani wanaumwa sana. Virusi hivyo ambavyo vinasambaa kwa njia ya maji maji mwilini, vinasababisha homa, kutapika, kuharisha na katika baadhi ya kesi mtu anavuja damu.

Kwa mujibu wa wizara ya afya Uganda, kuna Ebola za aina nne na kila moja imepewa jina la mahali iliporipotiwa kwa mara ya kwanza. Kuna Ebola Sudan, Ebola Zaire, Ebola Reston na Ebola Ivory Coast.

Mwanzoni mwa mwezi uliopita WHO ilitangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda ambao ulisababisha vifo vya watu 17. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, WHO ilisema ugonjwa huo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo umedhibitiwa baada ya kutokea vifo vya kesi 25.
XS
SM
MD
LG