Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:10

DRC yapata msaada wa Uingereza


Rais wa DRC Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alifanya ziara ya pamoja na mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa na mcheza sinema Angelina Jolie

Watu milioni 6 wakiwemo wathiriwa wa ubakaji watafaidika na huduma ya afya katika kipindi cha miaka 5 ijayo nchini DRC. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William
Hague alieko mjini Kinshasa amesema nchi yake imetoa msaada wa dola milioni 270 kwa ajili ya sekta ya afya nchini Congo.

Hague ambaye amefanya ziara ya siku mbili nchini DRC amekutana Jumatano na rais Joseph kabila na waziri mkuu Augustin Matata Ponyo.

Bw. Hague amefanya ziara ya pamoja nchini humo na mcheza sinema wa Hollywood, Bi. Angelina Jolie kukadiria hali ya wathiriwa wa ubakaji huko Kivu ya kaskazini. Waziri Hague amesema kwamba nchi yake ambayo itachukuwa uongozi wa G8 mwanzoni mwa mwezi April, na itafanya kila iwezalo kukomesha ubakaji nchini DRC.

Hague alisema “ nimezindua mpango mpya kuhusu huduma za afya kwa ajili ya wananchi wa Congo.Tutatoa msaada wa dola milioni mia mbili na sabini kwa ajili ya huduma hizo kwa ajili ya asilimia 10 ya jumla ya raia wa Congo”.

Kwa mujibu wa Bw. William Hague, msaada huo wa Uingereza kwa Congo unalenga ujenzi wa hospitali, ununuzi wa dawa na mafunzo ya wauguzi na madaktari,lengo kubwa likiwa kuwapa huduma bora za afya wahanga wa vita na ubakaji huko Kivu ya kaskazini na kusini.
Ziara hiyo ya William Hague na Angelina Jolie iliwapekeka mjini Kigali,Rwanda, Goma na Kinshasa nchini DRC.
XS
SM
MD
LG