Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:44

DRC: Beni yagubikwa na mikasa ya vita


Wanajeshi wa jeshi la Congo walikiwa msituni.
Wanajeshi wa jeshi la Congo walikiwa msituni.

Vita na mizozo vimezuka tena kuanzia katika mwa mwezi kwa kumi katika mji wa Beni nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya congo huku mamia ya watu wakipoteza maisha na maelfu kukoseshwa makazi yao.

Kwa mujibu wa mtetezi wa haki za binadamu Paluku Ngahangombi aliyoko katika mji huo na kushuhudia visa mbalimbali vinavyofanywa na wanaosadikiwa kuwa ni waasi wa ADF – NALU kutoka Uganda, anasema hali ya usalama inazidi kuwa mbaya.

Licha ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuanza kulala nje usiku wakiwasha moto, wakiwa na silaha kama vile mapanga na visu kujilinda na uvamizi wa waasi lakini bado ghasia zimeshamiri.

Usiku wa kuamkia Jumatano waasi walivamia kambi ya jeshi katika mji wa Beni kwenye mtaa mkubwa wa Owicha na kufyatuliana risasi na wanajeshi wa serikali hali iliyopelekea askari mmoja kupoteza maisha, na waasi wengi kujeruhiwa lakini waliweza kutoroka.

Wakazi wa mji huo wameilaumu serikali na Jeshi la umoja wa mataifa MONUSCO kushindwa kushirikiana vyema kurejesha hali ya utulivu .

Paluku Ngahangombi anasema kina mama na watoto ndio wahanga wakubwa katika mapigano na visa vinavyofanywa na waasi kwa sababu hawawezi kujikinga kwa haraka. Drc imegubikwa na vita, mizozo na mivutano ya aina mbalimbali kwa miongo kadhaa sasa.

XS
SM
MD
LG