Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 06:14

Mashauriano ya vyama vya Upinzani yakwama DRC.


 Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais Joseph Kabila anakabiliana na kibarua kigumu katika kuandaa mazungumzo ya kitaifa alioitisha wiki mbili zilizopita .Hiyo inatokana na mgawanyiko ulioko kwenye vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia nchini humo ambayo yanahisi kuwa hakuna haja ya mazungumzo ya kitaifa hivi sasa.Umoja wa mataifa umeingilia kati mazungumzo hayo ambayo yanahusu kuweko na taratibu ya uchaguzi wenye utulivu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:36 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Tarehe iliotolewa na rais Joseph Kabila ya kubuni tume ya maandalizi ya mazungumzo ya kitaifa ilimalizika Jumanne bila mafanikio yoyote. Kwenye taarifa iliotangazwa na kiongozi wa ofisi ya rais kupitia televisheni ya kitaifa ilisema kwamba, kubuniwa kwa tume hiyo kutafanyika hivi karibuni kwa ushirikiano na katibu mkuu wa umoja wa mataifa. Ban Ki Moon alietume mjumbe maalumu kukutana na upinzani,chama tawala na mashirika ya kiraia.

Hata hivyo wapinzani wengi wamesema hawatashiriki kwenye mazungumzo hayo wakidai ni njama ya rais Kabila na chama chake kuahirisha uchaguzi. Lakini baadhi ya vyama vya upinzani vimeunga mkono mazungumzo hayo.

XS
SM
MD
LG