Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:02

Donna Summer afariki kutokana na saratani


Mwimbaji Donna Summer
Mwimbaji Donna Summer

Mwimbaji huyo mashuhuru aliyejulikana kama Malkia wa Disco aliwafurahisha watu wa vizazi mbali mbali.

Donna Summer aliyeimba moja wapo ya nyimbo mashuhuri "Hot Stuff", aliweza kuwafurahisha watu miaka mingi baada ya kuacha mtindo huo wa Disco ulokua mashuhuri katika miaka 1970 na 1980.

Licha ya umashuhuri huo wote alionekana hakuwa na rahakuwa mashuhuri kwani alisema, wakati wowote mafanikio yanapopatikana basi inakua jambo geni."

Alizaliwa akiwa na jina la Donna Gaines hapo Disemba 31, 1948 mjini Boston, Massachusetts, na katika maisha yake aliweza kujinyakulia mara tano tunzo mashuhuri na kuu la muziki la Marekani Grammy.

kama waimbaji wengi mashuhuri wa Marekani wa makamu yake alinaza kuimba katika kwaya ya kanisa. Alipofika shule ya sekondari alianza tayari kucheza katika micehzo ya kuiga ya shule na wiki chache kabla ya nkuhetimu alikua katika mchezo wa kuigiza wa uwimbaji "Hair", jukumu lililompeleka hadi Ujerumani.

Huko Ujerumani alibaki kwa muda na mwajka 1974 akarikodi santuri yake ya kwanza, "Lady of the Night."

baada ya muziki wa Disco kutoweka Summer aliendelea kuimba na kuwatumubwiza mashabiki wake, hadi kufariki mapema Alhamisi katika jimbo la Florida ambako alikua anaishi na mumewe muimbaji Bruce Sudano

XS
SM
MD
LG