Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:34

Mshambulizi ya Boko Haram yapelekea ukosefu wa usalama wa chakula kukithiri Diffa, Niger.


Watu walopoteza makazi , karibu na Diffa, Niger.
Watu walopoteza makazi , karibu na Diffa, Niger.

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram, limewalazimisha takriban watu laki 3 kutafuta hifadhi katika eneo la Diffa kusini mashariki mwa Niger, eneo ambalo tayari linakabiliana na ukosefu wa usalama wa chakula ulokithiri. Mashirika ya kutoa misaada yanahangaika kutowa maji yakutosha na chakula kwa maelfu ya watu walotoroka mashambulizi mepya katika mji wa mpakani wa Bosso mwezi huu.

Kila siku ni mlolongo mkubwa wa watu wanaoshikilia madebe ya manjano, katika mojawapo ya mifereji iliopo huko Kidjendi, kambi iliopo takriban kilomita 40 Kutoka Diffa, kusini mashariki mwa Niger.

Cheldou Malou anaishi katika kambi na wanafamilia wake saba.

Malou anasema, kuna watu wengi. Mara nyengine wanaleta madebe mawili lakini wanajaza moja tuu. Ninakuja asubuhi, lakini sipati maji ya kutosha kwa hivyo nnarejea mchana.

Malou na familia yake ni miongoni mwa watu takriban elfu 50 walotoroka eneo karibu mji wa mpakani wa Bosso, kufwatia shambulizi la Boko Haram hapo Juni 3.

Wengi waliacha kila kitu nyuma na kutembea kwa siku kadhaa kabla kukusanyika katika kambi jangwani. Walijenga makazi kwa kutumia mikeka ya majani na plastiki zilogawiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali. Makazi hayo yako hatarini kupeperuka kila mara upepo unapovuma.

Watu walopoteza makazi huko Diffa Niger, wakisali chini ya makazi yalotengenezwa na majani.
Watu walopoteza makazi huko Diffa Niger, wakisali chini ya makazi yalotengenezwa na majani.

Kidjendi pekee ina wakimbizi takriban elfu 40, na watu walopoteza makazi.

Mkuu wa shirika la madaktari wasio na mipaka kitengo cha Uhispania huko Niger, Elmounzer Ag Jiddou, anasema hakuna maji ya kutosha.

Jiddou anasema, hali walio nayo kwa wakati huu inaweza kusababisha mizozo kwa sababu idadi ya maji wanaopata haitoshi, hasa kutokana na hali ya joto iliopo.

Siku chache zilizopita, mapigano kwenye kisima huko Kidjendi, yalipelekea mtu mmoja kufariki.

Baadhi ya wakulima walopoteza makazi waliweza kutoroka na mifugo yao, na sasa, ngombe na punda wanoranda kwenye kambi pia ni chanzo cha mivutano.

Chakula nacho kiko haba.

Yamgana Goni mkimbizi hapo Kidjendi alisema hakuna chakula wala makazi. Anasema, hamna chochote, na anahofu wanawe 9 watakufa na njaa.

Wafanyakazi wa kutowa misaada wanasema chanzo cha kutowa msaada bora ni kuwepo kwa usalama.

Lakini licha ya ongezeko la kijeshi, Boko Haram linaendelea kufanya mashambulizi ya hapa na pale katika eneo hilo, na hivyo watu wanaendela kuhama hama, na hivyo kufanya ugawaji wa misaada kuwa kugumu.

Diffa tayari ilikuwa na wakimbizi elfu 240 na na watu walopoteza makazi, pale mji wa Bosso uliposhambuliwa.

Mashirika ya kutowa misaada inaonya kuwa mzozo wa kibinadam huwenda ikaendelea katika eneo hilo kote katika eneo la ziwa chad.

XS
SM
MD
LG