Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:28

Wabunge zaidi kususia kuapishwa kwa Trump


Mbunge John Lewis, D-Ga., watatu kutoka kushoto akifuatana na wabunge wenzake azungumza na waandishi habari baada ya wa Democrats kumaliza malalamiko yao, June 23, 2016.
Mbunge John Lewis, D-Ga., watatu kutoka kushoto akifuatana na wabunge wenzake azungumza na waandishi habari baada ya wa Democrats kumaliza malalamiko yao, June 23, 2016.

Wabunge wapatao 23 wa chama cha Demokratik wametangaza hawatahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Donald Trump siku ya Ijuma.

Idadi hiyo ya wabunge iliongezeka mwishoni mwa wiki baada ya Trump kumkosoa, John Lewis, mbunge wa Atlanta, Georgia mwanaharakti mashuhuri wa kutetea haki za kiraia, alipohoji juu ya uhalali wa ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Novemba 8, 2016.

Katika mahojiano na kipindi cha "Meet The Press" cha kituo cha televisheni cha NBC, Lewis alisema kwamba kutokana na Rashia kuingilia kati na kujaribu kuhujumu utaratibu wa uchaguzi wa Marekani, hadhani uchaguzi wa Trump ni halali.

Mara moja Trump alijibu kupitia ujumbe wa tweeter akisema, "Mbunge John Lewis anglibidi kutumia wakati mwingi zaidi kutengeneza na kusaidia wilaya yake, ambayo iko katika hali mbaya na kuporomoka." akiendelea kusema badala ya kulalamika kuhusu matokeo ya uchaguzi angelifanya kazi na kuacha kuzungumza kuzungumza."

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mara mmoja matamshi hayo yamezusha hasira kutoka wabunge wa chama che Demokratik na baadhi ya Warepublican hawakuridhika pia ingawa wanashikilia kwamba Trump alichaguliwa kwa njia ya halali.

Mchambuzi wa masuala ya kisaisa Julius Nyangoro anasema kadhia hii imezusha hali ambayo haijawahi kushuhudia katika historia ya hivi karibuni, ya kipindi cha mpito cha kukabidhiana madaraka hapa Marekani.

Anasema Trump inaonesha hamfahamu vyema Lewis na vita alivyoviongozi tangu miaka ya 1960. Lewis alikamatwa mara kadhaa katika kampeni ya miaka 1960 ya kutetea haki za kiraia kando ya Mchungaji Martin Luther King, na hata kupigwa vibaya mwaka 1965 wakati wa maandamano ya Alabama.

XS
SM
MD
LG