Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:16

Kenya inakiuka kanuni za kimataifa kwa kufunga Daadab - Ripoti


FILE - Makao ya wakimbizi ya Dagahaley katika kambi ya Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.
FILE - Makao ya wakimbizi ya Dagahaley katika kambi ya Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinadamu, Huma Rights Watch, limesema leo Alhamisi kuwa uhamishaji wa wakimbizi kutoka kambi ya ya Daadab nchini Kenya unakiuka kanuni za kimataifa kwa sababu wengi wao wanaondoka na kurejea nchini kwao kutokana na uoga. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP.

Kenya imeelezea azima yake ya kufunga kambi ya Daadab kufikia mwezi Novemba, na kusema kuwa kambi hiyo ni tishio la kiusalama na ni gharama kubwa kwa raslimali ya taifa. Kambi hiyo inahifadhi takriban wakimbizi 266,000 kwa sasa.

Lakini Kundi hilo linasema kuwa baada ya kutembelea kambi hiyo mwezi jana, iiligundua kuwa raia wengi wa Somalia wanarejea makwao si kwa hiari yao, na kwamba wanakabiliana na hatari, dhuluma na njaa.

XS
SM
MD
LG