Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:11

CORD kupambana na Rushwa Kenya: Wetangula


Viongozi wa CORD, Raila Odinga (kulia) Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka
Viongozi wa CORD, Raila Odinga (kulia) Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka
Viongozi wa CORD nchini Kenya wamewataka wabunge wake kuimarisha juhudi zao kama chama cha upinzani na kufanya mabadiliko muhimu katika muelekeo wa nchi kwa wakati huu.

Viongozi wa CORD walikutana na wabunge na masenta katika mji wa Naivasha kwa mazungumzo ya siku mbili kujadili ajenda yao kuhusiana na masuala ya kuimarisha mfumo wa Ugatuzi, mabadiliko ya katiba, ufisadi na ulaji rushwa, pamoja na ugaidi nchini Kenya.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Moses Wetangula , moja wapo wa viongozi wa tatu wa mungano huo amesema wamezungumza na wabunge wao 129 na kuwapa muongozo wa chama watakapofungua bunge wiki hii.
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bw. Wetangula aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje anasema, "CORD ni muungano wenye nguvu , uloimarishwa na unamuelekeo unoaofaa, kwa sababu viongozi wake Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na mimi tumekubaliana ya kwamba miungano inayoundwa kwa haraka kwa ajili ya uchaguzi haidumu. Sisis tunataka muungano wetu uwe wa kudumu na mfano Kenya"

Akizungumza na waandishi habari kiongozi wa CORD Bw. Odinga, ametoa wito kwa wabunge wake kuwaondowa wajumbe wa tume ya uchaguzi akidai kwamba walishindwa katika uchaguzi ulopita kwa ajili ya uzembe wao katika kazi.

Wakati viongozi wa CORD walikua wanakutana Naivasha viongozi wa Jubilee walikutaka kwa mkutano wa faragha katika Ikulu ya Nairobi kujadili pia mikakati yao kabla ya kufunguliwa bunge.
XS
SM
MD
LG