Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:55

Zoezi la kuhesabu kura laendelea Congo


Rais wa Congo, Denis Sassou N'Guesso akipiga kura yake mjini Brazzaville, Congo, March 20, 2016.
Rais wa Congo, Denis Sassou N'Guesso akipiga kura yake mjini Brazzaville, Congo, March 20, 2016.

Kufunga mitandao ya mawasiliano si haki, na ni shambulizi kwa uhuru wa vyombo vya habari.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:41 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Zoezi la kuhesabu kura linaendelea huko Jamhuri ya Congo, lakini maelezo ni machache, huku serikali ikiwa imezuia matumizi ya simu na mitandao kote nchini. Rais Dennis Sassou Nguesso anatarajiwa kushinda kwa kiasi kikubwa muhula mwengine madarakani.

Jamhuri ya Congo iliitisha uchaguzi jumapili, huku ikiwa imekata mawasiliano na dunia .

Saa kadhaa kabla ya upigaji kura, serikali ya taifa hilo la afrika ya kati iliyataka makampuni ya simu na mitandao kufunga huduma kwa saa 48.

Shirika la Amnesty International ililaani hatua hio. Msemaji wa shirika hilo bi Allegozzi alisema, kufunga mitandao ya mawasiliano si haki na ni shambulizi kwa uhuru wa vyombo vya habari. Mamlaka lazima zihakikishe kuwa kila mtu anaweza kufanya shughuli zake bila hofu, bila manyanyaso.

Licha ya marufuku hio, mratibu wa muungano wa upinzani wa Congo aliweza kutuma ujumbe wa twitter jana na kuonyesha video ya watu wakisoma matokeo ya uchaguzi nje ya kituo cha kupiga kura.

Mawasiliano ya mtando yalizuiliwa mwaka jana pale maandamano dhidi ya kura ya maoni juu ya mabadiliko ya katiba ya kuongezaz umri na mda wa uwongozi wa rais. Kura hiyo ya maoni ambayo ilipita kwa asli mia 92, ilimruhusu Dennis Nguesso kuwania tena muhula mwengine, licha ya kuwa madarakani kwa mda wa iaka 32.

Uganda nayo ilichukuwa msimamo kama huo wa kuzuia mawasiliano wakati wa uchaguzi wao mwezi ulopita, na kufunga mitando ya kijamii kama vile twitter na Facebook, pale kura zilipokuwa zinapigwa na kuhesabiwa. Hata hivyo watu waliweza kutumia huduma ya VPN ili kuepuka marufuku hiyo. Matokeo rasmi yalimuonyesha mmoja wa marais walohudumu kwa mda mrefu barani Afrika, yoweri Museveni kashinda muhula mwengine madarakani.

Serikali ya Congo inasema marufuku ya sasa ya mawasiliano ni kujaribu kuzuia kutangazwa matokeo ya uchaguzi yasiyo rasmi.

Muungano mkuu wa upinzani ulibuni mfumo wao wa kuhesabu kura, wakidai tume rasmi ya uchaguzi ilipendelea upande mmoja tu, wa rais.

Umoja wa Afrika ulipeleka wafatiliaji mjini Brazzaville kwa uchaguzi wa jumapili, lakini umoja wa Ulaya haukufanya hivyo, wakisema hali za kuwepo uchaguzi ulo huru na wa haki haikutekelezwa.

XS
SM
MD
LG