Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:02

Kuwekeza kwa mwanamke ni jambo sahihi-Clinton


Hillary Clinton, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akizinduzi Siku ya Wanawake Duniani.
Hillary Clinton, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akizinduzi Siku ya Wanawake Duniani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton Jumatatu alizindua juhudi zinazojulikana kama “100 Women Initiative” ili kuwawezesha wanawake na wasichana kupitia mawasiliano ya kimataifa, wakati wa mkesha wa maadhimisho ya 100 ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.

Wanawake takriban 100 kutoka nchi 92 walikusanyika kwenye wizara ya mambo ya nje kuanza program ya wiki tatu ya kitaalamu nchini Marekani.

Waziri Clinton aliwaeleza washiriki kuwa kuwekeza kwa wanawake ni jambo sahihi na linaweza kusaidia kupunguza matatizo kama vile umaskini na njaa.
Aliwaita wanawake kuwa watu wa kujitolea katika biashara, taaluma,jamii za kiraia na serikali na amesema hatua zao zinamtia hamasa yeye na watu wengine.

Clinton alitambua mafanikio ya baadhi ya washiriki kama Raquel Fernandez kutoka Paraguay ambaye anajihusisha na wanawake na wasichana waliokumbwa na matatizo katika maisha. Huko nchini sudan, Aisha Humad ambaye anawawezesha wanawake kwa kuwapatia mafunzo ya kujikimu wenyewe na kupigania haki zao.

Wanawake wanashiriki katika program maalum inayojulikana kama International Visitor leadership, ambayo huwaleta kiasi cha watu 5,200 viongozi wa sasa na wanaoibukia hapa Marekani kujihusisha na wenzao wa Marekani na kufahamu maisha ya Marekani.


XS
SM
MD
LG