Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:34

Uchunguzi wa maoni unaonyesha ushindani mkali kati ya Clinton na Trump


Ushindani kati ya Hillary Clinton na Donald Trump unazidi kuongezeka.
Ushindani kati ya Hillary Clinton na Donald Trump unazidi kuongezeka.

Huku ikiwa imebaki chini ya wiki moja kufanyika uchaguzi nchini Marekani uchunguzi wa maoni unaonyesha ushindani mkali, Hillary Clinton na Donald Trump wanaingia kwenye gia za juu wakienda kufanya kampeni katika majimbo muhimu ili kuweza kushinda kuingia White house.

Mgombea wa Republikan Donald Trump alikuwa katika jimbo la Wisconsin jana Jumanne usiku na akiwataka wapiga kura wa chama cha Democrat ambao tayari wamekwishapiga kura zao za mapema kwa Clinton kuchukua fursa ya sheria ya upigaji kura wa mapema ya jimbo hilo kubadili kura zao.

Alitoa wito huo huo kwa wapiga kura katika majimbo mengine ambao amesema sasa wana majuto ya mnunuzi.

Katika kampeni yake katika jimbo jingine muhimu la Pennsylavania Trump amesema kama akichaguliwa ataitisha kikao maalum cha bunge kuondoa sheria ya mpango wa bima ya afya wa rais Obama uitwao Obama Care Trump amedai mpango huo wa bima ya afya ni janga na kuahidi kutoa mpango wake mwingine.

Rais Barack Obama alimpigia kampeni Hillary Clinton jijini Columbius Ohio Jumanne jimbo lingine ambalo kuna ushindani mkali.

XS
SM
MD
LG