Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 01:28

Clinton atoa mpango wake wa uchumi


Mgombea wa chama cha demokratik Hillary Clinton akizungumza kwenye mkutano wa kamp[eni huko Des Moines, Iowa, Ag. 10, 2016.
Mgombea wa chama cha demokratik Hillary Clinton akizungumza kwenye mkutano wa kamp[eni huko Des Moines, Iowa, Ag. 10, 2016.

Mgombea urais wa chama cha demokratik Hillary Clinton anatangaza mipango yake ya kiuchumi alhamisi akieleza kwamba mapendekezo yake ya kiuchumi yatawasaidia wafanyakazi wengi wa Marekani wakati yale wa mpinzani wake Donald Trump yatatoa punguzo la kodi kwa wamarekani matajiri kama yeye mwenyewe.

Clinton alizungumza katika kiwanda cha magari huko Detroit Michigan ambapo si mbali na pale Trump alipotoa wito wa punguzo kubwa la kodi kwa mashirika na watu binafsi nchini Marekani.

Wasaidizi wanasema Clinton waziri wa zamani wa mambo ya nje atapinga sera za uchumi za Trump na kusema kwamba ni za kuharibu uchumi wakati sera zake ni za kujenga na kuinua ajira na miradi mbali mbali ya umma kukarabati madaraja, barabara na viwanja vya ndege.

Katika mkutano wa hadhara huko Iowa alisema mpango wake utaongeza ajira milioni 10 na kusema kwamba mpango wa Trump utaleta hasara kwenye soko la ajira kwa kupoteza zaidi ya ajira milioni 3.

XS
SM
MD
LG