Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:09

Clinton aanza ziara barani Afrika


Waziri wa mambo ya nje wa Marejani Hillary Clinton alipozungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa Ukimwi Washington Dc.
Waziri wa mambo ya nje wa Marejani Hillary Clinton alipozungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa Ukimwi Washington Dc.

Clinton anafanya ziara Afrika kuhamasisha maendeleo ya ukuaji uchumi na demokrasia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton anaanza ziara ya Afrika Jumanne, Senegal ikiwa nchi ya kwanza katika ziara yake ya siku 10 barani humo ambayo pia itamfikisha Kenya na Uganda ili kuhamasisha maendeleo ya ukuaji uchumi na demokrasia.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema Clinton atakutana Jumatano na rais mpya wa Senegal Macky Sall na kuonyesha nchi hiyo kama mfano wa uvumilivu wa taasisi za kidemokrasia.

Bw.Sall alimshinda rais wa zamani Abdoulaye Wade katika uchaguzi wa Machi baada ya mabishano kuhusu Bw.Wade kugombea urais kwa muhula wa tatu.

Clinton atatembelea pia Sudan Kusini ikiwa ni taifa jipya la Afrika kufuatia kujitenga kwake na Sudan mwaka jana. Ziara yake inaingiliana na mdahalo wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa juu ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kumaliza mzozo unaoendelea wa mafuta, uraia na mipaka kati ya nchi hizo mbili.

Clinton anatarajiwa kuelezea miradi ya Marekani juu ya HIV/UKIMWI, elimu na maendeleo wakati wa ziara yake. Nchi nyingine atakazotembelea Waziri Clinton ni pamoja na Malawi na Afrika Kusini.

Waziri Clinton amefanya safari kadhaa siku za nyuma Afrika kusini mwa jangwa la Sahara . Mwaka jana alitembelea Ethiopia, Zimbabwe na Tanzania.

XS
SM
MD
LG