Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:03

Clinton: Afrika inahitaji mshirika sio mfadhilii


waziri wa mambo ya nchi za nje Hillary Clinton akitoa chandarua cha kukinga umbu alipokitembelea kituo cha afya Dakar
waziri wa mambo ya nchi za nje Hillary Clinton akitoa chandarua cha kukinga umbu alipokitembelea kituo cha afya Dakar
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, aliianza ziara ya siku kumi ya nchi za Afrika huko Dakar, kwa kusema Afrika inahitaji ushirikiano na sio mfadhili .
“Wakati wote wa ziara yangu Afrika wiki hii, nitazumgumzia juu ya mfano wa ushirikano endelevu unaoongeza thamini badala ya kuiondoa. Hiyo ni dhamira ya marekani kwa Afrika.”

Clinto alizumgumza kwenye chuo kikuu cha Cheikh Ante Diop baada ya kukutana na Rais wa Senegal Macky Sall. Bwana Sall alichaguliwa Machi kufuatia mapambano na maandamano kupinga serikali na uchaguzi uliokuwa na mashindano mkali ulopelekea kipindi cha mpito cha amani cha kukabidhi madaraka kwa njia ya kidemokrasia.
Waziri Clinton aliipongeza Senegal kama bingwa wa demokrasia na rafiki wa kweli wa Marekani.

“ Kama kuna anayeshuku ikiwa democrasia inaweza kustawi barani Africa, basi waache waje Senegal. Wamerkani wanaihusudu Senegal kama nchi pekee Afrika Magharibi ambayo haijakuwa kamwe na mapinduzi ya kijeshi.”

Hata hivyo, waziri huyo alibainisha kwamba nchi mbili jirani, Mali na Guinea-Bissau zinaonyesha kuna kazi nyingi inayohitajika kufanywaa kwatika bara hilo. Nchi zote mbili zinapambana kurudi katika hali ya kawaida ya kikatiba baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka huu.

Clinton anasema mapinduzi ya wananchi Kaskazini mwa Africa yameonyesha kuwa “Njia za kale" za uongozi hazikubaliwi tena na kwamba viongozi ambao wanashikilia madaraka kwa ajili ya kujitajirisha binafsi, wako upande mbaya wa historia.

Waziri Clinton ana ratiba yenye kazi nyingi mnamo siku kumi zijazo, akizitembelea Sudan Kusini, Uganda, Kenya na Afrika Kusini. Hii itakuwa ziara yake ya kwanza Afrika tangu utawala wa Obama ulipozindua mkakati wake mpya kwa Afrika mwezi Juni.

Sera hiyo ina nguzo nne: kuimarisha taasisi za kidemokrasia, ukuaji wa uchumi, biashara na uwekezaji; kudumisha amani na usalama na kukuza maendeleo.
Afrika ni miongoni mwa mabara yenye uchumi unaokuwa kwa haraka pamoja na idadi ya wakazi duniani na bi. Clinton alisisitiza kwanini ushirikiano na Marekani itakuwa kwa maslahi yao kya muda mrefu.
XS
SM
MD
LG