Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:38

Benki ya Dunia yasifu hatua za India


Mtoto wa Jammu, India, June 12, 2015.
Mtoto wa Jammu, India, June 12, 2015.

Rais wa Benki ya Dunia, Jim Kim, alisema leo Jumatano akiwa ziarani India kwamba nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya utapia mloo wakati wa utotoni lakini bado nchi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi.

Chini ya asilimia mbili ya watoto wa India wana kile Benki ya Dunia inachosema ni mahitaji ya msingi wakati wa utoto wao na miaka muhimu ya maisha: haki ya chakula, huduma bora ya afya, fursa ya kujifunza mapema na maji safi.

Japokuwa Benki ya Dunia inasema India ipo kwenye njia ya kukabiliana na utapiamlo wa watoto chini ya miaka mitano, inasema tatizo ni kwamba program za India zinaelekezwa kwenye watoto wa shule za chekechea na kukosa muda muhimu wakati wa siku 1,000 za maisha ya mtoto pale ukuaji unapoanza.

XS
SM
MD
LG