Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:30

Je unaweza kupata saratani kwa kutumia sana simu ya mkono


Mkulima nchini Kenya anatumia simu ya mkono
Mkulima nchini Kenya anatumia simu ya mkono

Uwezekano wa kupata ugonjwa wa saratani kwa kutumia sana simu ya mkono

Utafiti mkubwa kuwahi kufanywa hadi leo juu ya kupima madhara ya afya kutokana na kutumia simu za mkono, umeamua kwamba vyombo hivyo haviongezi hatari ya kupata saratani ya ubongo miongoni mwa watumiaji wa kawaida wa simu za mkono. Hata hivyo umegundua kuwepo na hatari kidogo miongoni mwa watumiaji wakuu.

Mradi huo mkubwa wa utafiti wa kimataifa uliofanywa na kitengo cha utafiti wa utumiaji simu cha Shirika la Afya Duniani, uliwachunguza zaidi ya watumiaji simu za mkono 13,000 katika nchi 13 mnamo muongo uliopita. Kwa ujumla wanachama wa tume walieleza kwamba nishati ya miyale ya radio inayozalishwa na simu hizo haiongezi hatari katika aina mbili kuu za uvimbe wa ubongo. Yaani glioma na meningioma.

Hata hivyo wakati watafiti walipochunguza matokeo ya asilimia 10 ya watu ambao walijieleza kua ni watumiaji wakuu wa simu waligundua muongezeko wa asilimia 40 katika hatari ya kupata uvimbe wa glioma. Watumiaji wakuu ni pamoja na wale ambao wanazungumza kwenye simu za mkono angalau kwa nusu saa kwa siku, siku saba katika wiki, kwa muda wa miaka 10.

Lakini mjumbe mmoja wa jopo, Daniel Kewski kutoka taasisi ya kutathmini hatari za afya kwa wakazi, The Centre for Population Health Risk Assessment, kutoka chuo kikuu cha Ottawa nchini Canada, anasema kundi halikuweza kuthibitisha kuwa watumiaji wa mara nyingi wa simu za mkononi waliongeza hatari ya saratani kwa sababu utafiti ulikua chini ya misingi ya kumbukumbu zisizo za uhakika za baadhi ya washiriki.

Kewski anasema asilimia 90 ya watumiaji walobaki walikuwa kwenye kiwango cha kutumia chombo kwa wastani wa saa mbili mpaka saa mbili na nusu kwa mwezi.

Otis Brawley, daktari mkuu na mwanasayansi wa shirika la saratani la Marekani, American Cancer Society, anasema kuna ushahidi mdogo kwamba hata watumiaji wakubwa wa simu za mkononi unasababisha muongezeko mkubwa wa kupata saratani ya ubongo. Na kama ilisababisha, anasema Brawley, tatizo litakuwa limegubikwa na matatizo menginre makubwa zaidi ya afya ya jamii.

Ripoti ya tume ya Interphone Study Group, juu ya utumiaji wa simu za mkono na hatari za saratani ya ubongo ilichapishwa na jarida la International Journal Of Epidemiology.

XS
SM
MD
LG