Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:55

Uchaguzi C.A.R. wahairishwa hadi Jumatano

Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Africa ya kati (C.A.R.) inafanya matayarisho ya mwisho mwisho ya uchaguzi baada ya kuhairishwa kwa zoezi hilo ambalo awali lilipangwa kufanyika siku ya Krismasi.
Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Africa ya kati (C.A.R.) inafanya matayarisho ya mwisho mwisho ya uchaguzi baada ya kuhairishwa kwa zoezi hilo ambalo awali lilipangwa kufanyika siku ya Krismasi.

Na BMJ Muriithi, VOA

Tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Africa ya kati (C.A.R.) inafanya matayarisho ya mwisho mwisho ya uchaguzi baada ya kuhairishwa kwa zoezi hilo ambalo awali lilipangwa kufanyika siku ya Krismasi.

Huku zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi huo ambao sasa utafanyika siku ya Jumatano, wananchi wengi pamoja na jamii ya kimataifa wana matumaini kwamba zoezi hilo litaleta amani kwa taifa ambalo limekumbwa na vita kwa muda wa miaka mitatu.

Siku tano tu kabla ya uchaguzi huo wa rais na wabunge, kadi za kupigia kura ziliwasili katika mji wa Boeing unaopakana na mji mkuu wa Bangui, hayo ni kulingana na shirika la habari la AFP.

Kadi hizo ziliwasili mjini Bangui siku ya Jumatano, hali ambayoilipelekea kikosi cha kulinda Amani nchini humo (MINUSCA) kutoweza kuzisafirisha kwenye mikoa tofauti kwa wakati uliofaa, na kupelekea kusitisshwa kwa matayarisho ya kupiga kura siku ya Ijumaa kama ilivyopangwa.

Wafanya kazi wa tume ya uchaguzi walionekana wakipanga kura hizo kwa haraka haraka.

“tunajaribu kuzipanga kulingana na majina yanavyofuatana kialfabeti," alisema Andre Gamtan, msimamizi wa kituo cha kupigia kura mjini Boeing.

Mzozo wa kisiasa uliibuka pale waasi walipomng’oa mamlakani rais Francois Bozize mnamo mwaka wa 2013 na kupelekea umwagikaji wa damu katika taifa hilo.

Lakini Roland Marchal, ambaye ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa wa shule ya Kidplomasia ya kimataifa huko Paris Ufaransa, ametoa tahadhari na kusemasema kwamba uchaguzi uliotayarishwa kwa haraka huanda usilete suluhu kwa mzozo nchini humo, na badala yake huenda ukachangia kuzorota kwa hali ilivyo sasa.

XS
SM
MD
LG