Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:25

Carson:Waislam hawafai kuwa Rais wa Marekani


Mgombea urais wa Republican, Dr. Ben Carson katika mdahalo wa pili wa Republican, Sept. 16, 2015.
Mgombea urais wa Republican, Dr. Ben Carson katika mdahalo wa pili wa Republican, Sept. 16, 2015.

Mgombea urais wa Republican, Ben Carson alisema Jumapili kwamba waislam hawafai kuwa Rais wa Marekani, akidai kwamba misingi ya ki-Islam haiendani na thamini za Marekani. “Sitatetea tumuweke muislam kuwa kiongozi wa taifa hili. Kwa hakika sikubaliani na hilo”, Carson, mkristo mcha mungu alizungumza kwenye kipindi cha Meet the Press katika televisheni ya NBC nchini Marekani.

Alisema imani ya rais ni jambo la kuangaliwa na wapiga kura na alielezea kwamba imani ya ki-Islam haipo ndani ya katiba, japokuwa hakufafanua kwa njia ipi uislam hauendani na misingi ya katiba.

Matamshi ya Carson yamekuja kufuatia swali la papo kwa papo alilokataa mgombea wa Republican, Donald Trump wiki iliyopita kutoka kwa mtu mmoja, ambaye wakati wa tukio la kampeni katika jimbo la New Hampshire, kwa makosa alimuita Rais Barack Obama ni muislam na alisema waislam ni tatizo katika nchi hii.

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump

Trump na gavana wa jimbo la Ohio, John Kasich wagombea wanaopingana wa Republican pia walionekana katika matukio tofauti kwenye vipindi vya NBC.

Kasich aliulizwa iwapo atakuwa na tatizo na muislam akiwa White House.“Jibu mwishoni mwa siku, utatakiwa kufuata kanuni na watu watakuangalia kila wakati, alisema. Lakini kwa mimi jambo muhimu kuhusu kuwa rais ni kwamba una ujuzi wa uongozi, unajua unachokifanya na unaweza kusaidia kutatua tatizo katika nchi hii na kuiongoza nchi hii. Hizo ndizo sifa ambazo mimi nazijali.”

Alipoulizwa iwapo Muislam ataweza kuchaguliwa, Trump alisema “baadhi ya watu wanasema tayari imeshatokea”.

Mgombea urais wa Republican, Ben Carson
Mgombea urais wa Republican, Ben Carson

Wakati Carson alipoulizwa kama anaamini Obama ni mkristo, alisema “ninaamini ni mkristo. Sina shaka yoyote na kile anachokisema”.

Katika mahojiano mbali mbali siku ya Jumapili, Trump alijaribu kutenganisha kati ya wa-Marekani wote waislam na waislam wenye msimamo mkali nchini Marekani na kwingineko.

XS
SM
MD
LG