Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:17

Mazungumzo ya kuleta amani Burundi kufanyika Julai 12-14


Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, anayeongoza mazungumzo ya amani ya Burundi.
Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, anayeongoza mazungumzo ya amani ya Burundi.

Duru nyengine ya mazungumzo yanayolenga kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Burundi kwa njia za amani, yatafanyanyika Julai 12 mjini Arusha Tanzaznia.

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa, yatahudhuriwa pia na waday wa kisiasa wa Burundi, na yanalengwa kumaliza mzozo wa kisiasa uliopelekea warundi zaidi ya laki moja na nusu kutoroka nchini mwao, na mamia wengine kuuwawa.

Serikali ya rais Pierre Nkuruzinza bado ingali ikishikilia msimamao uleule, wa kukataa kuja kwenye meza moja ya majadiliano na wale ambao inasema walihusika na vurugu zilizofanyika nchini humo.

Mkutano huo unatarajiwa kuendelea kwa mda wa siku tatu utaanza Julai 12 hadi 14.

Rais wa zamani Benjamin Mkapa alichaguliwa kuwa mpatanishi wa utaratibu huo na viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, mnamo mwezi Marchi mwaka huu.

Duru ya kwanza ya mazungumzo yalifanyika Arusha hapo mwezi Mei.

XS
SM
MD
LG