Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 04:02

Burundi yasema ipo tayari kwa mashauriano ya kisiasa ya nchi hiyo


Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi
Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Nyamitwe alisema nchi yake ipo wazi kwa mashauriano na nchi au kundi lolote katika nchi kuhusiana na mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Bwana Nyamitwe alisema serikali ya Rais Pierre Nkurunziza inataka amani na demokrasia nchini Burundi pamoja na ushirikiano wa umoja wa Ulaya-EU. Lakini alisema mashauriano yeyote hayawezi kuwa tishio au kuhukumu.

Mkutano wa Jumatatu wa mawaziri wa EU mjini Luxembourg ulituma barua kwa serikali ya Burundi ikitaka yafanyike mashauriano kwa kile inachokiita kutoheshimu kanuni za mkataba wa Cotonou, ambao unaongoza maendeleo ya kiuchumi na mahusiano kati ya EU na mataifa ya Afrika, Caribbean na Pacific. Mkataba wa Cotonou unaorodhesha “utawala bora” kama “nyenzo muhimu”, ukiukaji ambao unaweza kupelekea kufungiwa baadhi ya maeneo ya maendeleo ya ushirikiano au kufunguiwa kabisa.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akisalimiana na wananchi
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akisalimiana na wananchi

EU hivi karibuni ilielezea wasi wasi kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Burundi na utata wa kuchaguliwa tena kwa Rais Pierre Nkurunziza, hatua ambayo wakosoaji wake wanaiita ukiukaji wa katiba ya Burundi. Kwa mujibu wa ripoti serikali ya Burundi ina muda wa siku 30 za kujibu barua hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, bwana Nyamitwe alisema serikali yake itajibu baada ya kuipokea barua hiyo.

XS
SM
MD
LG