Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 11:38

Mazungumzo ya Burundi bado hali tete.


Wanachama wa National Front of Liberation Agaton Rwasa na Leonce Ngendawmana katika mazungumzo ya amani.
Wanachama wa National Front of Liberation Agaton Rwasa na Leonce Ngendawmana katika mazungumzo ya amani.

Mazungumzo ya Burundi ambayo yameanza rasmi jana huko Kampala Uganda yanaelekea kukutana na vikwazo hasa baada ya serikali ya Burundi kutoa taarifa na kukosoa vikali maandalizi ya kikao hicho.

Akizungumza na sauti ya Amerika mchambuzi wa siasa za Uganda Akol Amazima anasema serikali ya Burundi imeingia kwenye mazungumzo hayo na mtazamo hasi na duru za kisiasa nchini humo zinaitaka jamii ya kimataifa isilegeze kamba juu ya mzozo huo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mazungumzo hayo yako chini ya upatanishi wa rais Yoweri Kaguta Museveni. Serikali ya Burundi kupitia taarifa iliyosaniwa na mkuu wa ujumbe wa serikali katika kikao cha Jumatatu jijini Entebe waziri wa mambo ya nje Alain Nyamitwe inalaani kile walichosema mpatanishi alialika makundi ambayo hayatambuliwi na sheria za Burundi.

Kundi hilo ni muungano wa wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa kiraia wanaodai kutetea hadhi ya makubaliano ya Arusha ambao walitoroka nchi baada ya kudhihirisha upinzani wao dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Vile vile serikali ya Burundi inasema kuwa hawakubaliani juu ya muendelezo wa mazungumzo hayo ambapo baada ya uzinduzi jijini Uganda vikao vitaendelea jijini Arusha Tanzania tarehe 6 januari.

XS
SM
MD
LG