Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:26

Umoja mataifa yahofia Burundi kuingia tena kwenye mzozo


Vikosi vya Burundi
Vikosi vya Burundi

Mchunguzi maalum wa umoja umataifa anaonya kuwa Burundi huenda ikatumbukia tena kwenye vita, kama jumuiya ya kimataifa haitachukua hatua za haraka kuzuia hilo.

Pablo de Greiff, mchunguzi maalum wa umoja mataifa kwa ukiukaji mkubwa, anasema mengi yametokea tangu alipoitembelea Burundi mwezi December, na hamna lilo zuri. Anasema ,Burundi imejiondoa kwenye njia ya amani ambayo imeifuata tangu mwaka 2000, pale makubaliano ya Arusha yalipomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Anasema serikali ya rais Pierre Nkuruzinza haijaribu tena kujenga jamii kutokana na kanuni za sheria, na kwamba utamaduni wa kutokhifia kushtakiwa kutoka miongo iliyopita umejikita zaidi na unatumiwa kama nyenzo ya ukandamizaji na ghasia.

De Greiff anasema amewasilisha wasiwasi wake kwa baraza la haki za binadam la umoja mataifa kwa matarajio nchi kuwa nchi wanachama watafahamu ukubwa wa hali inayojitokeza nchini Burundi na kuchukuwa hatua ili kuepuka janga kutokea.

De Grieff anasema, anataka kuwa muwazi, na kujaribu kutowa wito wa haraka na wito wa tahadhari kwa jumuiya ya kimataifa, wasisubiri hadi tufikwe na janga jingine mikononi mwetu kabla ya kuchukuwa hatua.

Takriban watu laki 3 waliuwawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi.

Taifa hilo lilikuwa na Amani katika miaka ya karibuni hadi mwishoni mwa mwezi Aprili, pale rais Nkuruzinza alipotangaza kuwania muhula wa tatu madarakani. Tangu wakati huo, De Greiff anasema, kumekuwepo na Zaidi ya mauwaji mia 1, mamia ya ukamataji holela na kesi nyingi za mateso na kutendewa vibaya.

Anasema hamna kesi inayochunguzwa ila moja inayohusisha afisa wa serikali.

Rais alichaguliwa tena mwezi July, lakini mivutano bado ipo baina ya wafuasi wake na wale wanaosema amekiuka katiba ambayo imeweka kiwango cha mihula miwili tu kwa rais kuwepo madarakani.

Mchunguzi huyo wa umoja mataifa anasema jumuiya ya kimataifa na serikali za kikanda haziwezi kumudu kukaa na kusubiri ukatili mpya utokee tena nchini Burundi. Anaonya kuwa hii inahatarisha mzozo mkubwa kuweza kutokea katika eneo la maziwa makuu, na matokeo ambayo yanatisha na yasiyojulikana.


XS
SM
MD
LG