Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:05

Bunge la Uganda lapitisha mswada wa adhabu kwa mashoga


Washiriki katika maadhimisho ya siku ya wapenzi wa jinsia moja Entebbe, Uganda mapema mwaka huu.
Washiriki katika maadhimisho ya siku ya wapenzi wa jinsia moja Entebbe, Uganda mapema mwaka huu.
Bunge la Uganda Ijumaa lilipitisha mswada ambao utafanya baadhi ya vitendo vya ngono kati ya watu wa jinsia moja kupewa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:03 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mswada huo awali ulishtumiwa na makundi ya kutetea haki pamoja na serikali za Magharibi ikiwemo Marekani kwa sababu ulijumuisha adhabu ya kifo.

Mswada uliopitishwa Ijumaa unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa yeyote atakayehukumiwa kwa kile ilichosema ni "vitendo vilivyopita mipaka" vya ngono kati ya watu wa jinsia moja.

Waziri Mkuu Amama Mbabazi alikaririwa akisema kuwa serikali ya Uganda itafanya mashauriano zaidi kuhusu mswada huo ambao unahitaji kutiwa saini na Rais Yoweri Museveni kabla ya kuwa sheria kamili nchini humo.
XS
SM
MD
LG