Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:01

Boko Haram imezidisha matumizi ya watoto kama wajitoa mhanga


Rebecca Issac, mwanafunzi wa Chibok ambaye alikimbia kutoka kwa kundi la Boko Haram, anazungumzia yaliyomsibu kwenye mikono ya kundi hilo la wanamgambo.
Rebecca Issac, mwanafunzi wa Chibok ambaye alikimbia kutoka kwa kundi la Boko Haram, anazungumzia yaliyomsibu kwenye mikono ya kundi hilo la wanamgambo.

Wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria wameongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya watoto kama walipuaji wa mabomu wa kujitoa mhanga.

Hii ni kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF. Ripoti iliyotolewa na shirika hilo leo Jumanne inasema kwamba watoto wapatao 44 walihusika katika visa vya Boko Haram vya ulipuaji mabomu wa kujitoa mhanga mwaka uliopita, hii ikiwa ni mara kumi ya visa vilivyoripotiwa miaka minne kabla ya hapo.

Kulingana na ripoti hiyo, kwa kipindi cha miaka miwili sasa, mmoja kati ya watu watano waliojilipuua kwa kujitoa mhanga ni mtoto, na asilimia sabini na tano kati ya hao ni wasichana. Kundi hilo la kigaidi limekuwa likiwatumia watoto, wengi wao wakiwa hawana habari kwamba wamebeba vilipuzi, kwenye maeneo ysokoni na sehemu zenye watu wengi, kama vile misikitini, ambako ni vigumu kushukiwa kwamba ni walipuaji wa kujitoa mhanga.

XS
SM
MD
LG