Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:23

Besigye awasilisha malalamiko kwa mwanasheria mkuu wa Uganda


Kiongozi wa upinzani wa Uganda Dr. Kizza Besigye akiwahutubia wafuasi wake huko Uganda.
Kiongozi wa upinzani wa Uganda Dr. Kizza Besigye akiwahutubia wafuasi wake huko Uganda.

Mgombea urais wa zamani wa chama cha Forum for Democratic Change-FDC cha nchini Uganda, Kizza Besigye, amemwandikia mwanasheria mkuu nchini humo malalamiko kuhusu kile anachokiita kutotendewa kwake haki.

Bwana Besigye ambaye anadai alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika februari 18, mwaka huu alifunguliwa mashtaka ya uhaini baada ya video moja kuonesha kwamba alikuwa akiapishwa na chama chake kama rais wa Uganda.

Katika barua yake Besigye alirudia kuelezea kutotendewa kwake haki na serikali na mfumo wa sheria nchini humo zaidi ya miaka kadhaa kuanzia ushiriki wake katika uchaguzi wa urais mwaka 2001. Alisema amekuwa akikandamizwa mara kwa mara na kupewa kikwazo cha uhalali wa kuwania nafasi ya urais.

XS
SM
MD
LG