Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:32

Benki ya Dunia yasaidia pembe ya Afrika


Baadhi ya watoto nchini Somalia ambao wanataabika na utapiamlo kutokana na baa la njaa lililoikumba nchi za eneo la Pembe ya Afrika- Julai 18, 2010
Baadhi ya watoto nchini Somalia ambao wanataabika na utapiamlo kutokana na baa la njaa lililoikumba nchi za eneo la Pembe ya Afrika- Julai 18, 2010

Benki ya Dunia imetangaza msaada wa dola milioni 500 kusaidia waathirika wa ukame katika nchi za eneo la pembe ya Afrika.

Rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick alisema katika taarifa ya Jumatatu kwamba ni muhimu kuchukua hatua haraka ili kuepusha janga la kibinaadam.
Fedha hizo zitasaidia kote miradi ya muda mfupi na mrefu katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zinajumuisha Kenya, Djibouti, Ethiopia na Somalia ambayo sasa imekumbwa na baa kubwa la njaa.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 11 katika eneo hilo wanahitaji msaada wa haraka. Maelfu ya watu tayari wamekufa kutokana na njaa na wengi zaidi wanataabika kutokana na utapiamlo.

Benki ya Dunia imeahidi kutoa msaada huo wa fedha kufuatia mkutano wa dharura na Umoja wa Mataifa huko Rome juu ya matatizo ya ukame.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pia linaarifiwa juu ya hali hiyo mbaya ya upungufu wa chakula nchini Somalia wakati wa mkutano wa faragha mjini New York, Jumatatu.

Umoja wa Mataifa umetangaza hali mbaya ya upungufu wa chakula katika maeneo ya Bakool na Lower Shabelle nchini Somalia, maeneo yote ni ngome ya kundi la wanamgambo wa al-Shabab wenye ushirika na kundi la kigaidi la al-Qaida.
Makundi ya kutoa misaada ya kibinadamu yanasema yanapata taabu kupeleka misaada katika maeneo hayo kwa sababu ya vitisho vya kundi la al-Shabab.

Kundi hilo la al-Shabab liliweka marufuku kwa makundi mengi ya kigeni ya kutoa msaada kuingia katika eneo lao na linakanusha kwamba maeneo yaliyo chini yake yanataabika na ukosefu wa chakula.

Shirika la afya Duniani-WHO linasema maeneo matano zaidi katika mji wa kusini mwa Somalia yameathiriwa mno na uhaba wa chakula.


XS
SM
MD
LG