Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amependekeza karibu kikosi cha askari 12,000 wa kulinda amani wa umoja wa Afrika kupelekwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo vurugu za kidini hazionyeshi dalili za kudhibitiwa .
Katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu Bw.Ban alisema jukumu la kwanza la jeshi hilo litakuwa kulinda raia.
Bw.Ban aliwahi kusema siku za nyuma kwamba ana wasiwasi ghasia hizo za Jamhuri ya Afrika ya Kati huenda zikasababisha migawanyiko nchini humo.