Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:24

Ban Ki Moon atowa wito wa kuongezwa majeshi ya AMISOM Somalia.

Spika wa bunge la Somalia Sharif Hassan Sheik Aden, (Kushoto) na rais wa Somalia Sheik Sharif Sheik Ahmed, wakisalimiana na katibu mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki Moon huko Mogadishu.
Spika wa bunge la Somalia Sharif Hassan Sheik Aden, (Kushoto) na rais wa Somalia Sheik Sharif Sheik Ahmed, wakisalimiana na katibu mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki Moon huko Mogadishu.

Ban Ki Moon awa katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa mataifa kutembelea Somalia kwa zaidi ya miaka 18 akisema ziara hiyo ni ya kuimarisha usalama.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema walinda amani wa kimataifa wamesaidia serikali ya Somalia kupata mafanikio makubwa ya usalama huko Mogadishu lakini amesema wanahitaji kuongeza wanajeshi zaidi ili kudumisha usalama katika maeneo mengine ya nchi.

Bw. Ban alitoa maelezo hayo jana baada ya ziara fupi huko Somalia , ikiwa ni ya kwanza kufanywa na mkuu wa Umoja wa Mataifa katika zaidi ya miaka 18. Alisema ziara hiyo yake ni ishara ya kuimarisha kwa hali ya usalama.

XS
SM
MD
LG