Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:14

Umoja wa Afrika AU kupigia kura tume mpya leo


 Mwenyekiti anayeondoka wa umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini Zuma
Mwenyekiti anayeondoka wa umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini Zuma

Mkutano wa umoja wa Afrika unaofanyika mjini Kigali utapigia kura tume mpya ya Umoja huo hii leo, licha ya uvumi wa mwito wa uchaguzi huo kuahirishwa.

Kumekuwa na uvumi unaoendelea kwenye mkutano huo kwamba nchi wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, hazijafurahishwa na chaguo la wagombea walopendekezwa kuchukuwa nafasi ya mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika anayeondoka, Bi Nkosozana Dlamini Zuma.

Kuna wagombea watatu, wawili kati yao ni wanawake, makam rais wa zamani wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe na waziri wa mambo ya nje wa Botswana Pelonomi Venson Moitoi, na waziri wa mambo ya nje wa Equitorial Guinea, Agapito Mba Mokury.

Jana jioni, mshauri wa kisheria wa Umoja wa Afrika, Vincent O Nmehielle, alikanusha uvumi wa kucheleweshwa huko.

Nmeheielle alisema, acheni kushuku. Hakukuwa na wasiwasi wa ECOWAS ulofanya uchaguzi uakhirishwe. Uchaguzi utafanyika leo. Hakuna majina mengine yataingizwa kwenye orodha wakati uchaguzi ukiendelea. Iwapo kwa namna fulani itashindikana kupata wingi wa kura unaohitajika, basi sheria zitafwata mkondo na mtashuriwa juu ya matokeo.

ECOWAS haiamui iwapo uchaguzi wa tume ya Au utafanyika, anasema Bw. Nmehielle.

Sheria za AU zinaeleza kuwa mgombea anaeshinda lazima apate theluthi mbili za kura za wanachama. Nmehielle anaeleza kuwa iwapo hakutakuwepo na mshindi katika duru ya kwanza, mgombea mwenye kura kidogo ataondolewa na duru ya pili ya uchaguzi itafanyika.

Iwapo theluthi mbili bado hatizitopatikana, basi uchaguzi utaaghirishwa hadi uchaguzi mwengine ufanyike na mwenyekiti wa mpito kuchaguliwa.

Mwandishi mmoja alihoji sifa za kidemokrasia za nchi za baadhi ya wagombea. Nmehielle alikataa kujibu.

Bw. Nmehielle aliuliza, unaweza kunifafanulia demokrasia? Unaposema wagombea kutoka nchi zisizo za kedemokrasi, sifahamu nini unachomaanisha. Wao ni wanachama wa Umoja wa Afrika. Ili kuwa mgombea nafasi iko wazi kwa wanachama wote wa umoja wa Afrika.

Kwa mujib wa sheria za umoja wa Afrika mwenyekiti wa tume hiyo na naibu wake wanachauliwa na viongozi wan chi wanachama au wawakilishi wao katika mkutano huo, wakati makamishna wanane wanachaguliwa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama.

XS
SM
MD
LG